Ijumaa , 15th Feb , 2019

Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Hamidu Bobali amedai alishawahi kuwashawishi viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa akijiunga na chama hicho atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 200.

Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Hamidu Bobali.

Kauli hiyo ameitoa mapema jana katika mkutano wa Jumuiya Vijana Chama Cha Wananchi CUF uliofanyika visiwani Unguja ambapo pia ilishuhudia Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hammad akishiriki.

Bobali ameeleza kuwa viongozi wa CCM walimwambia wangeweza kumpa nafasi nyingine kwenye uongozi wa Chama cha Mapinduzi, madai ambayo Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM ameyakataa.

Amesema ujasiri ndio uliomfanya ashinde majaribu hayo, akibainisha kuwa mbali na mamilioni hayo aliyoahidiwa, pia aliahidiwa kuwa atateuliwa kuwa Naibu Waziri.

Aidha Mbunge huyo amesema kilichomfanya ashindwe kujiunga na CCM ni utu na uzalendo huku akiwashangaa wabunge wa upinzani waliohamia CCM kwa maelezo kuwa wamewasaliti wananchi waliowachagua.