Ijumaa , 15th Feb , 2019

Mbunge mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu 'Sandwich' katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia.

Darij Krajcic.

Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo na walikua wakiendelea na shuguli zao na hakujulikana kama ameiba lakini baadae baadhi ya wanachama walisisitiza arudi kulipa pesa ya mkate huo.

''Nilisimama pale kwa dakika tatu, nikitaka wanihudumie,", alijitetea Mbunge huyo.

Krajcic ameomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya, baada ya suala lake la kuiba kusambaa baada ya kuwaambia wabunge wengine wakati wa mkutano wa kamati siku ya Jumatano ambapo siku ya Alhamisi spika wa bunge hilo Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.