Jumatatu , 22nd Apr , 2019

Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia amewataka wapiga kura wake, kutowaamini watu wanaozusha maneno kwamba ametaka kuhamishia ujenzi wa hospitali ya Wilaya Mkunwa badala ya Nanguruwe.

Rais Magufuli

Akizungumza na wananchi wa Nanguruwe, Ghasia amesema kwamba yeye mwenyewe alipata taarifa kuwa Baraza la Madiwani wamehamisha Hosptali ya wilaya Mtwara, isijengwe Nanguruwe na wameipeleka Mkunwa wakidai kuna maelekezo toka Tamisemi ingawa hawezi kuwalaumu.

"Kuna wengine wanaozusha kwamba eneo la Mkunwa ni la Hawa Ghasia, Jamani! Ghasia ana maeneo mangapi? uko mnakosikia wanasemaje kwamba mimi ndo nalazimisha wajenge Mkunwa nilipwe fidia? Msidanganyike. Niko na nyinyi kuhakikisha maagizo ya Rais Magufuli yanatekelezwa" Mbunge Ghasia

Ameongeza kwamba "Kabla ya Rais kufika hapa.Nilipata taarifa kuwa Baraza la Madiwani wamehamisha Hosptali ya wilaya Mtwara,isijengwe Nanguruwe na wameipeleka mkunwa wakidai kuna maelekezo toka Tamisemi. Nikaenda Tamisemi wakakataa. Siwalaumu Madiwani,wamedanganywa".

Pamoja na hayo, Mbunge Ghasia amesema kwamba "Tangu nimekuwa Mbunge sijawahi kuwa na mkutano mkubwa kama huu. Ndugu zangu wa Nanguruwe tukitaka tushinde hii vita mimi  na nyinyi tuwe kitu kimoja, tukianza kugombana wenyewe tutashindwa na ndo wanachotaka. Hakuna anayeweza kubadili agizo la Rais, Hospitali itajengwa hapa