Jumatano , 15th Jan , 2020

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa ofisi yake inaendelea kuratibu mipango ya mazishi ya Mbunge wa Newala Vijijini, Rashid Akbar, aliyeaga Dunia leo Januari 15, 2020, Mingoyo mkoani Lindi.

Mbunge Rashid Akbar wakati wa uhai wake, kulia na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Spika Ndugai amepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa na kutoa pole kwa wanafamilia wote.

"Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo familia ya marehemu, Waheshimiwa Wabunge, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu" amesema Spika Ndugai.

Aidha kwa upande wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara, kupitia kwa Katibu wa Siasa na Uenezi mkoani humo, kimetoa taarifa za pole kwa wale wote walioguswa na msiba wa Mbunge huyo.