Jumanne , 10th Mar , 2020

Kuelekea hukumu ya kesi ya viongozi wa CHADEMA leo, Mbunge wa Kawe Halima Mdee ametoa ujumbe wa kuwaaga watu.

Mbunge wa Kawe Halima Mdee

Halima ameandika maneno kupitia Ukurasa wake wa Twitter, akiwa ameambatanisha na picha yake akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe pamoja na wanawake wengine wanachama wa BAWACHA.

Viongozi wanane wa Chadema pamoja na katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo ya kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na kusababisha woga na hofu kwa wakazi wa Kinondoni na kifo cha Akwelina Akwilini.

Viongozi hao ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika. Wengine ni naibu katibu mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) na mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee (mbunge wa Kawe); Ester Bulaya (Bunda); John Heche (Tarime Vijijini).