Jumanne , 1st Sep , 2020

Waziri wa Katiba na Sheria, ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Dkt Mwigulu Nchemba, amesema kuwa miongoni mwa wagombea wanaojinadi kama ni watoto wa Singida siyo wazalendo kwa kuwa kuna mmoja alipokuwa Waziri alikuwa anaenda kunyosha Suti nje ya Nchi.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Mwigulu Nchemba.

Dkt Nchemba ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 1, 2020, katika Uwanja wa Bombadier uliopo Mjini Singida, wakati mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiomba kura kwa wananchi wa Mkoa huo.

"Wengine wanakuja hapa wanajifanya eti ni watoto wa Singida hawana hata uzalendo, kuna mmoja Mh Rais tulikuwa Mawaziri wote hata Suti zake alikuwa anaenda kunyoosha Ulaya, anauchungu na Singida huyo!, wengine walikuwa wanasema Tanzania siyo salama sasa hivi wamekuja sababu advance wamechukua baada ya uchaguzi tu watasema siyo salama", amesema Dkt Nchemba.

Aidha Dkt Nchemba ameongeza kuwa, "Ninyi Wana Singida niwaambieni Rais ni huyu Dkt Magufuli na kwa kuwa sisi ndiyo mtakuwa mnatutuma, niwaombe ihurumieni Tanzania wale wagombea wengine wote nawafahamu na nikiangalia janja janja yao hata advance walishachukua nchi yetu itauzwa".