Alhamisi , 3rd Dec , 2020

Mfanyabiashara mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwalimu Juma, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na  shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 3.14

Mfanyabiashara huyo, amefikishwa mahakamani hapo  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Ruboroga.

Akisomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali, Neema Mushi, amedai, Oktoba 17, mwaka huu eneo la Azam Marine wilaya ya Ilala jijini Dar-es-Salaam, mshtakiwa alikamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin.

Baada ya kusomewa  shtaka hilo Hakimu Ruborogwa, amesema kuwa mshtakiwa huyo  haruhusiwi kujibu chochote kwa sababu Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

Baada ya kusema hayo mtuhumiwa amerudishwa rumande na kesi hiyo itatajwa tena Desemba 8 mwaka huu.