Jumapili , 23rd Sep , 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema baadhi ya pesa zitakazopatikana katika michango ya Watanzania zitatumika kujenga uzio na mnara katika makaburi ya watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Akizungumza katika shughuli ya mazishi leo Septemba 23,2018 visiwani Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza amesema baadhi ya miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo fedha hizo hazitatumika katika shughuli yoyote nje ya tukio hilo.

"Fedha hizi ni za wafiwa hivyo hatuna budi kuzitumia kulingana na mwenendo wa tukio tutafanya ukarabati wa kutosha katika baadhi ya vivuko ikiwemo Mv Misungwi, Sengerema ili kuimarisha usafiri wa majini katika maeneo yote”, amesema Majaliwa.

Amesema ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo hawapati tabu Serikali iko katika mkakati wa kuleta kivuko cha muda na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa tume ya uchunguzi itaundwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na serikali ikiwa tayari iko katika mazungumzo juu ya matumizi ya Meli ya Mv Nyahunge.

Kivuko cha MV. Nyerere mpaka sasa takwimu zinaonyesha kilikuwa na watu 265 ambao kati yake 224 wamepatikana wakiwa tayari wamepoteza maisha huku 41 wakipatikana wakiwa hai.