Ijumaa , 9th Sep , 2022

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, ametoa siku 14  kwa maafisa elimu ndani ya mkoa huo kuorodhesha migogoro yote ya ardhi inayohusisha uvamizi wa maeneo ya shule ili serikali iweze kuitatua.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla

RC Makalla ametoa agizo hilo leo Septemba 9, 2022, wakati wa uzinduzi wa miongozo na mikakati ya elimu kwa mkoa huo huku akitaka Wakurugenzi wa Halmashauri kutoa fedha kwa shule zote kuwe kwa mipaka ili kupunguza migogoro ya wavamizi.

RC Makalla ametaka mchango wa walimu kuheshimiwa, na changamoto zao kusikilizwa na kutatuliwa huku akitaka suala la wanafunzi kupewa chakula shuleni kutazamwa vizuri kwani lina manufaa makubwa 

RC Makalla amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia miongozo, pamoja na kutatua changamoto zitakazojitokeza huku Wakuu wa wilaya wakiahidi kufanyia kazi maagizo waliyopewa.