Jumatano , 19th Jun , 2019

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro, amewaonya askari wake kuwa wasiwe kikwazo kwa wafanyabiashara nchini ili kuhakikisha wafanyabiashara hao wanakuwa waadilifu kwenye suala la ulipaji wa kodi.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Maofisa na Wakaguzi wa jeshi hilo ambapo amesema kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa askari anayeshiriki kwenye matukio yatakayoikwamisha nchi.

"Lengo kubwa ni kufanya tathmini kwa miaka 2 iliyopita tumefanya nini na hatufaanya nini, pia nimesisitiza sana sisi hatuwi vikwazo kwa wafanyabiashara kwa sababu mishahara yote tunayolipwa inatokana na kodi za wafanyabiashara", amesema IGP Sirro.

"Suala la weledi ni muhimu sana lazima ujue mbinu za medani za kivita, lazima ujue kupeleleza na mapambanao ya silaha ni lazima tulipeleke jeshi vizuri, kwa sababu tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa tunahakikisha unaenda vizuri, pia kwa uchaguzi wa 2020 lazima tuanze maandalizi leo," ameongeza.