Jumapili , 26th Mei , 2019

Naibu Waziri Vijana Anthony Mavunde ameupongeza uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Dar es salaam kwa kuja na mkakati wa Ubungo ya kijani ambao unalenga chama hicho kurejesha baadhi ya maeneo ambayo yanaongozwa na vyama vya upinzani.

Kubenea akiwa na Mnyika.

Maeneo hayo ni Jimbo la Ubungo linaloongozwa na Saed Kubenea na jimbo la Kibamba linaloongozwa na John Mnyika.

Mavunde ametoa kauli hiyo wakati akizindua kampeni ya Ubungo ya kijani ambayo iliyoanzishwa na jumuiya hiyo ya vijana ya CCM kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza kwenye Uzinduzi huo, Mavunde amesa kuwa, "mambo maazuri sharti yaigwe, nampomgeza Mwenyekiti Wa CCM mkoa, Musa Kilakala kwa kuja na mkakati Wa Dar es salaam ya kijani ili kurejesha maeneo yote kuwa chini ya CCM, kiongozi yeyote anapimwa kwa maono yake, Mkoa wa Dar es salaam mmetisha sana kuleta suala hili kuwa sehemu kubwa ya vijana ili kurejesha majimbo ya Ubungo na Kibamba".

"Simuoni Kubenea wala Mnyika wakichomoka kwenye kampeni hii ya Ubungo wa kijani, tujitahidi ndugu zangu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye mitaa 91, tuhakikishe tunashinda yote kwenye uchaguzi mdogo", ameongeza Mavunde.