Jumanne , 5th Nov , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaan, Paul Makonda, amesema kuwa angekuwa na uwezo wa kutunga sheria angeweka utaratibu ambao hautamtoza faini yoyote dereva wa gari atakayekwangua bampa la gari ya mtu mwingine.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Hayo ameyabainisha leo Novemba, 5, 2019, alipotembelea watoto wanaopatiwa matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo, Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) na kuwaomba watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kuokoa uhai wa watoto wenye uhitaji.

"Mimi ningekuwa na uwezo wa kutunga sheria, binafsi ningesema mtu akikukwangua bampa achana naye tu wewe shuka kwenye gari angalia bampa yako, mwambie pole kwasababu wala hukukusudia.", amesema Makonda.

"Kuna watu mkiguswa tu bampa ya Vits au Ist mnabaki mpaka msongamano wa magari unakuwa mkubwa, ukiguswa kidogo kama gari yako haijaharibika msamehe tu mwenzio.", ameongeza Makonda.

Aidha Makonda amesema kuwa anataka kuufanya mwezi Disemba kuwa ni wa shukrani kwa kuwainua watoto wenye matatizo ya moyo wanaopitia maumivu makali huku wakiwa hawana tumaini lolote la kupona na kuwapeleka katika viwango vingine.