Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James
Akizungumza katika Mkutano wa baraza kuu la UVCCM linalofanyika jijini Dodoma amesema ni muhimu kulinda staha ya kila chama na wagombea ili umoja na mshikamano katika Nchi yetu uendelee.
“Sisi tunaapa mbele ya watanzania wote umoja wa vijana utakuwa wa kwanza kulinda na kuyaenzi maadili ya uchaguzi na hivyo tunawasihi wenzetu kupitia taasisi na asasi zingine wafanye hivyo, wakifanya kinyume chake sisi tutailinda nchi yetu na tutakilinda chama chetu na viongozi wetu’’- amesema James.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa leo ni siku ya kihistoria kwao kama vijana baada ya kuaminiwa na Chama kwa mara nyingine na kupewa nafasi ya kutafuta wawakilishi wao katika vyombo vya maamuzi na kudai kuwa haki imerudi ili kupimwa kama vijana hao ni waadilifu.
Aidha amesema umoja wa Vijana wa UVCCM ndiyo tanuru la hoja na kwamba ndio msingi wa viongozi imara wa leo na kesho.