Jumamosi , 23rd Jun , 2018

Mlipuko mkubwa umetokea katika mkutano wa Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed  ambapo mtu mmoja amefariki na wengine 154 kujeruhiwa.

Waziri Mkuu Abiyamelielezea shambulio hilo kuwa shambulio ambalo halikufanikiwa lililofanywa na nguvu ambayo haitaki kuona Ethiopia ikiungana. 

Waziri wa Afya nchini humo Amir Aman ametoa taarifa kwa njia ya Twitter ambapo amesema watu 9 wapo katika hali ya mahututi kati ya majeruhi 156 .

Wakati wa tukio hilo Bw. Abiy ilibidi aondoshwe kwa haraka eneo la tukio muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake wakati mlipuko huo.

Maelfu ya wananchi walikuwa wamekusanyika katika bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa katika mkutano ulioandaliwa kuiunga mkono serikali yake Abiy ambaye ni mrithi wa aliyekuwa waziri mkuu Haile Mariam aliyejiuzulu Februari mwaka huu.