Ijumaa , 7th Feb , 2020

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa tayari wanamshikilia kijana aliyejulikana kwa jina la Daniel Maleki, aliyeonekana kwenye video fupi akichana na kuitemea mate Quran Tukufu.

Kijana Daniel Maleki akichana Quran

Akizungumza leo Februari 7, 2020 Kamanda Mutafungwa amesema kuwa baada ya upelelezi kufanyika tayari kijana huyo amekwishafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kilosa na kusomewa mashtaka ya kuudhi na kukashfu dini.

"Mtuhumiwa baada ya kufikishwa kituoni alihojiwa kwa kina na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo ukawa umeafanyika na leo amefikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kilosa na kushtakiwa kwa kosa la kufanya kitendo cha kuudhi na kukashifu imani ya kidini" amesema ACP Mutafungwa.

Video hiyo fupi imesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ikimuonesha kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa ni Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kitengo cha Biashara, akichana kitabu cha Dini ya Kiilsamu, Juzuu Amma ambayo ni sehemu ya Quran Tukufu.