Ijumaa , 11th Sep , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Claudia Kitta amesema kuwa wamefanikiwa kuwaokoa wagonjwa wote pamoja na baadhi ya samani na vifaa tiba vya Hospitali ya Kyela iliyoungua moto mchana wa leo.

Hospitali ya wilaya ya Kyela ikiteketea kwa moto

Moto huo umezuka mapema leo Septemba 11, 2020, ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo chanzo cha moto hakijajulikana, na uchunguzi umekwishaanza ili kubaini chanzo na athari zilizojitokeza.

Imeelezwa kuwa moto huo umezuka majira ya saa 7:00 mchana ukianzia kwenye wodi ya watoto, ambapo ulifanikiwa kuzimwa majira saa 9:00 mchana kutokana na nguvu za wananchi waliojitokeza hospitalini hapo na haujaleta madhara yoyote kwa binadamu.