Mpina ataka ipandishwe bei ya ununuzi wanyama

Jumatatu , 16th Apr , 2018

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya nyama ya punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao kutoka shilingi laki mbili ya sasa ili kudhibiti utoroshaji wa mifugo hiyo kwenda nje ya nchi.

Akizungumza mara baada ya ziara yake katika kiwanda cha nyama ya punda cha Hua Cheng nje kidogo ya mji wa Dodoma, Waziri Mpina amesema kuwa bei hiyo ya sasa haiendani na gharama halisi ya ufugaji wa punda ndio sababu wafugaji hutorosha mifugo hiyo na kukosesha taifa mapato.

"Inakadiriwa zaidi ya punda 10,000 hutoroshwa mipaka kwa siku kwenda nje ya nchi wanakonunuliwa kwa bei ya juu ambapo ni sawa na zaidi ya punda milioni moja kwa mwaka hivyo kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 32 kama ushuru na takribani bilioni 24.21 za kodi ya mapato ambayo yangepatika katika nyama ambayo ingeuzwa nchini",amesema Waziri Mpina.

Katika hatua nyingine Waziri Mpina ameunda tume ya watalaam kutoka wizarani kufanya tathmini kama kiwanda hicho kimetimiza masharti yote yaliyotolewa na serikali baada ya kukifungulia adhabu Februari mosi mwaka huu