Jumapili , 22nd Sep , 2019

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania na wanajumuiya wa Afrika Mashariki, kupenda tamaduni zao na kuachana na tamaduni za watu wengine.

Samia ameyasema hayo leo Septemba 22, 2019, wakati wa uzinduzi wa matamasha mawili ya utamaduni likiwemo la Urithi Festival na JAMAFEST, na kusema kuwa utamaduni umekuwa ukitufundisha mambo mbalimbali ikiwemo kufanya kazi kwa bidii.

"Tamaduni zetu zinatufundisha mambo mengi sana mathalani kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, kulinda na kuheshimu utu, na mtu yeyote asiyeuthamini utamaduni wake huyo ni mtumwa wa tamaduni nyingine." amesema Mama Samia.

Akizungumzia suala la ubunifu wa kazi za mikono Mama Samia amesema, ubunifu wa  kazi za mikono za  zinazofanywa vijijini, hususani vile vikapu vinavyotengenezwa mkoani Iringa, vinafanya vizuri zaidi katika soko la nchini Finland.