Mtangazaji Nguli afariki dunia

Alhamisi , 18th Oct , 2018

Aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Radio One na ITV, ambaye baadaye alijiunga na Idhaa ya kiswahili ya Radio Deutch Well ya Ujerumani(DW) Isack Gamba ameekutwa amefariki dunia mjini Bonn Ujerumani.

Isack Muyenjwa Gamba.

Taarifa za kifo cha Isack Gamba zilijulikana baada ya kutofika kituo chake cha kazi, ambapo inadaiwa kuwa amekutwa amefariki nyumbani kwake leo Alhamisi Oktoba 18, 2018.

Mmoja kati ya mfanyakazi mwenzake amesema kuwa taarifa zilizotoka nchini Ujerumani zinasema kuwa Gamba hakuonekana kazini kwa muda wa siku mbili, Jumanne na jana Jumatano Oktoba 17.

Amesema kuwa leo pia hakuonekana kazini asubuhi, ndipo watu wa ofisini wakaenda kutoa taarifa polisi, waliofika nyumbani kwake na kuvunja mlango wakamkuta Gamba amefariki tayari.