Alhamisi , 23rd Mei , 2019

Naibu Waziri wa Mawasiliano Atashasta Nditiye, amebainisha kuwa Wizara anayoiongoza inamshikilia mtu mmoja (jina halijatajwa), ambaye anatuhumiwa kumiliki laini za simu zinazokaribia 600.

Naibu Waziri wa Mawasiliano Atashasta Nditiye

Naibu Waziri Nditiye amebainisha hayo leo, Mei 23, 2019, nje ya vikao vya Bunge jijini Dodoma alipokuwa akizungumzia juu ya mwenendo wa zoezi la usajili wa laini unaoendelea hivi sasa kupitia Makampuni ya simu.

"Kuna watu wana laini nyingi sana, tumemkamata mtu juzi ana laini 629, kwenye takwimu zetu za watu milioni 40 wanaotumia laini za simu, si ajabu watu milioni 3 wamejilimbikizia laini za simu." amesema Naibu Waziri Nditiye.

Zoezi la usajili wa laini kwa njia ya kieletroniki kwa sasa linaendelea nchi nzima, ambapo zoezi hilo limeanza Mei Mosi mwaka huu.

Kwa sasa Serikali inakataza mwananchI kutumia laini 2 za mtandao mmoja, bila ya kuwa na kibali kutoka kwa TCRA.