Ijumaa , 13th Dec , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mtemi Msafiri, amesema anamsaka Mmoja wa Watendaji wa Kijiji wilayani humo, kwa madai ya kuwakeketa watoto wake na kwamba akikamatwa atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mtemi Msafiri.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa ufunguzi wa kambi okozi kwa ajili ya mabinti, wanaokimbia ukeketaji na kukimbilia Katika kambi ya ATFGM Masanga.

"Sheria zipo na lazima tuzisimamie, niwaambie nimepata habari kuna Mtendaji mmoja wa Serikali amekeketa watoto wake na tumemfuata bahati mbaya hatukuwakuta watoto wake, tunasubiri wakirudi tu tunamkamata" amesema DC Msafiri.

Aidha Msafiri ameongeza kuwa "Niseme tu mila zozote zinazoenda kinyume na sheria za nchi, lazima tuzisimamishe, kama kuna kiongozi yeyote wa Serikali, anashiriki mambo hayo mnieleze naenda kumkamata".