Mtoto wa Sokoine afariki dunia

Wednesday , 18th Oct , 2017

Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Tanzania marehemu Edward Moringe Sokoine, Kereto Sokoine amefariki dunia kutokana na ajali aliyoipata nyumbani kwake mkoani Arusha.

Akiongea na kipindi cha East Africa Drive kinachorushwa na East Africa Radio, kaka wa marehemu ambaye ndiye msemaji wa familia, Lemblis Kipuyo, amesema kifo hicho cha marehemu kimesababishwa na ajali aliyoipata alipokuwa akitaka kuruka geti kuingia nyumbani kwake, tofauti na taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi mkoani humo, kwamba alikuwa akigombana na mkewe.

Msikilize hapa chini akisimulia jinsi kifo hicho kilivyotokea.