Ijumaa , 18th Mei , 2018

Mansa Musa ndiye mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani. Kina Bill Gates na matajiri wa dunia unaowajua hajawahi kufika rekodi ya utajiri wake. Mansa Mussa Alikuwa Mfalme Wa Mali kuanzia mwaka 1312 hadi mwaka 1337.

Alizaliwa mwaka 1280 na lipewa jina la "Mansa" likimaanisha mfalme wa wafalme, sababu alitawala ufalme mkubwa Afrika, uliojulikana kama "Malike Empire" au Mali Empire. Babu yake Mansa Musa alikuwa kaka wa Sundiata Keita ambaye alianzisha 'Mali empire'.

Anashikilia rekodi ya kuwa mtu tajiri zaidi kuwahi kutokea duniani ambapo utajiri wake umetajwa kuwa dola za kimarekani bilioni 400, ambazo kina Bill Gates na hata tajiri namba moja wa sasa Jeff Bezos, hawjahi kufikia, kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg Billionaires Index

Wakati wa utawala wake alikuwa akimiliki dhahabu zenye thamani kubwa. Aliwahi kufanya safari ya kihistoria ambapo alipeleka Hija watu 60,000 kwa mpigo! na kuwasafirisha watumwa 12,000 kwa ajili ya ibada hiyo takatifu kwenye dini ya Kiislam, huku akisafiri kwa kutumia ngamia zaidi ya 100 ambao wamebeba dhahabu zenye kilo zaidi ya 100 kila mmoja.

Imeelezwa kwamba alikuwa na desturi ya kujenga misikiti kila ijumaa, na baadhi ya misikiti aliyoijenga ni pamoja na Msikiti mkubwa wa Djingareyber ambao upo mpaka leo, na umewekwa chini ya Urithi wa dunia na UNESCO.

Msikiti wa Djinguereber uliopo huko Timbuktu Mali, ambao ulijengwa na Mansa Musa