Jumamosi , 15th Dec , 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango, amethibitisha kuharibika kwa takribani nyumba 157 kwenye wilaya yake, baada ya kunyesha kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

Mvua ikinyesha

Mkuu huyo wa Wilaya amesema licha ya kuharibika kwa nyumba za wananchi, pia majengo ya serikali pamoja na Zahanati yamekumbwa na uharibifu huo, ambapo mvua hiyo ilipiga zaidi ya kata tatu.

Ametaja maeneo yaliyokumbwa na upepo huo katika Kata za Stesheni kuwa ni jumla ya nyumba na Zahanati 83, Kata ya Songambele nyumba 14 na kata ya Nachingwea nyumba 60 na kufanya idadi kufikia 157.

Hata hivyo, bado haijafahamika hasara iliyopatikana na ofisi yake imewaagiza wataalamu kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini thamani yake. Mvua hiyo inatajwa ilianza kunyesha majira ya saa 10:30 hadi saa 11:30 jioni.