Jumatatu , 21st Oct , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo, amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo,kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya iliyopo kata ya Kaengesa, wilayani Sumbawanga Dastan Mlelwa, anafikishwa mahakamani

 

haraka iwezekanavyo, baada ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili.

Wangabo amesema kuwa licha ya Mwalimu huyo kujisalimisha Polisi, lakini ipo haja ya vyombo vya usalama mkoani humo, kuhakikisha vinafuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha anachukuliwa sheria stahiki.

 “Hili jambo hatutalifumbia macho, Mkuu wa shule kuwatafuta wanafunzi kimapenzi na mpaka kuwatia mimba, yeye kama mzazi na mwalimu haikubaliki hata kidogo, huu ni ubakaji kwasababu wale wanafunzi wa kidato cha pili na cha tatu hawana umri wa miaka 18 ni chini ya hapo, ni ubakaji,” amesema Wangabo.

 

Katika hatua nyingine Wangabo, amewaagiza wajumbe hao wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa, kufuatilia kesi ya wizi wa mifugo inayomhusisha Afisa mifugo wa mji mdogo wa laela, wilayani humo Emanuel Tluwey, baada ya kukamatwa akiwa anachinja ng’ombe wa wizi.