Mwanafunzi  akutwa ameuawa shambani

Ijumaa , 15th Mar , 2019

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Yungwe wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita, Alex Pastory amekutwa ameuwawa kwenye eneo la kichaka  huku sababu za kifo hicho zikiwa bado azijajulikana.

Kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjori Mwabulambo

Akizungumza na  Waandishi wa  habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masono aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukerewe kwaajili ya matibabu kutokana na hali ya afya yake kutokua nzuri.

Amesema,marehemu alipewa ruhusa na kuondoka kwenda nyumbani na alivyo maliza matibabu February 28   mwaka huu alirejea shuleni na kuendelea na masomo yake.

Aidha,Kamanda Mponjoli amesema tangu Machi mosi mwezi huu mwanafunzi huyo  alitoweka shuleni pia hakuonekana katika maeneo ya nyumbani ambapo alikua amepanga.

Sanjari na hayo, Kamanda amesema ilipofika tarehe 8 mwezi huu mama mmoja ambaye jina lake halikujulikana, wakati akiwa shambani analima aliona fuvu la binadamu kwenye eneo la shamba lake hali iliyomshitua na kupelekea kuwaita wananchi na walipofika na kuchunguza walibaini kuwa ni mabaki ya nguo za shule kuwepo kwenye eneo hilo.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.