Jumatatu , 24th Sep , 2018

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani Juma Aweso amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza umakini wa hali ya ulinzi katika jimbo lake la Pangani kufuatia kifo cha dereva wa bodaboda aliyefahamika kwa jina la Sharo.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani Juma Aweso (kushoto) na marehemu Sharo aliyekuwa dereva wa bodaboda, (kulia).

Kupitia ukurasa wake wa kijamii Naibu Waziri Juma Aweso ameonesha kuguswa na kifo cha kijana huyo ambaye inatajwa alikua dereva wa bodaboda wilaya Pangani na  anadaiwa kunyongwa na watu wasiojulikana na kumuibia pikipiki.

Naibu Waziri Aweso ameandika “Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kifo cha kijana mwenzangu maarufu kwa jina la Sharo kilichotokea kwa kunyongwa jimboni Pangani..,Nikiri kua jambo hili limenigusa na kuniumiza sana,nimepeleka hisia zangu mbali na kuwaza kijana asie na hatia anayehangaika kufanya kazi kutimiza malengo yake anakatizwa uhai wake kwa ajili ya wizi wa pikipiki na kupoteza maisha,ama kwa hakika inasononesha sana…”

Nitoe wito kwa serikali tena kwa hisia kali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kuliangalia suala hili kama jambo la dharula na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu kwani sio mara ya kwanza inatokea.” Aliongeza Naibu waziri Aweso