Jumatano , 19th Feb , 2020

Mbunge wa Vunjo kupitia Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia, amesema kuwa chama hicho kilipambana kuleta hoja mpya ya elimu ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanikiwa na Serikali kupitisha hoja ya K tatu yaani Kusoma, Kuandika na Kuhesabu huku wakitaka kuongeza K ya nne.

Mbunge wa Vunjo kupitia NCCR Mageuzi, James Mbatia

Hayo ameyabainisha leo Februari 19, 2019, jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho na kusema kuwa hoja yao ya msingi kwa sasa ni kuwa na ushirika wa pamoja wa kuwa na Katiba shirikishi kwa Watanzania wote.

"Sisi NCCR tulikuwa na hoja ya elimu tuliizungumza, tulipambana katika hoja siyo kwa ngumi kuhusu kurudishwa kwa K tatu, Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, leo hii tunahoja ya kuwa na K ya nne ya kusikiliza, tuna udhaifu mkubwa sana wa kutokusikiliza msikilize mwenzako anasema nini na kuwa na mawazo shirikishi" amesema Mbatia.

Aidha Mbatia akizungumzia sula la kurudi CCM amesema kuwa hana mpango wowote wa kuvaa shati lenye rangi ya kijani, kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amemsaliti mama yake mzazi aliyeasisi chama hicho.