Ijumaa , 13th Dec , 2019

Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400, inatarajiwa kuwasili nchini Disemba 14, 2019, na itapokelewa jijini Mwanza.

Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400.

Jana Disemba 13, akizungumza  kwenye Kikao ca Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mwenyekiti CCM ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, alisema ndege hiyo imeachiwa.

"Kwanza kwa taarifa tu Ndege yetu iliyokuwa imeshikwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa tarehe ya kuipokea na mtaipokea hapa hapa Mwanza" amesema Rais Magufuli.

Novemba 23, 2019, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alisema Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400, imekamatwa nchini Canada, na aliyesababisha ndege hiyo kushikiliwa ni yuleyule, Hermanus Stayn raia wa Afrika Kusini, aliyekuwa amefungua kesi na kusababisha ndege ya Tanzania aina ya Airbus A220-300 kushikiliwa nchini Afrika kusini, Agosti mwaka huu.