Jumatatu , 4th Feb , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amerejea nchini akitokea kwenye matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu alipokuwa amelazwa nje ya nchi.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipokuwa amewasili Ommy Dimpoz amesema haamini kama amerudi nyumbani licha ya watu mbalimbali kumzushia kuwa amekufa.

Ommy Dimpoz amesema, "hali kama unavyoiona mimi mwenyewe siamini naona nimefika nyumbani, kiukweli kuhusu uzushi wa kifo nishazoea kwa sababu ya kazi niliyoichagua inatufanya tuzoee hali kama hii."

"Lakini wanachojisahau duniani wote tunapita kila mtu atakufa na mimi nitakufa, kuhusu kuanza kuimba kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote." ameongeza Ommy Dimpoz.

Msanii huyo kwa kipindi kirefu amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya koo baada ya kusemekana kula chakula chenye sumu hali ambayo ilimfanya afanyiwe upasuaji Afrika Kusini na Agosti 2018 ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa msanii huyo kueleza mbele ya umma juu ya ugonjwa wake