Jumatatu , 21st Oct , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, ameeleza kushangazwa na baadhi ya watanzania kuwa wafuasia wa baadhi ya watu ambao, wamekuwa wakisambaza taarifa zisizo na ukweli kwa nia ovu huku wengine wakieendelea kusifiwa.

Makonda ameonesha hali hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Baba Keagan, ambapo amesema ni jambo la ajabu kuona watu wanaosambaza uongo, ndiyo watu ambao wanafuatiliwa sana kwenye mitandao.

"Nilitarajia kungekuwa na kampeni kabambe ya kulaani wazushi, waongo na waovu, ila cha ajabu ndiyo kwanza wanasifiwa, mbona tunaendelea kuwafuata kwenye mitandao? Mbona “hatuwaunfollow? tunataka kujifunza nini kutoka kwao?." ameandika Makonda.

"Tanzania tumeshaingia katika hii hatari hivi inawezekanaje mtu anazusha habari mbaya za mwingine hata kumtakia kifo je kikitokea anapata faida gani? inawezekanaje watu kuinuka na kutetea wanaoharibu maadili ya jamii yetu?Taifa tunaelekea wapi?" ameongeza Paul Makonda.