Jumatatu , 20th Jan , 2020

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, limefanikiwa kuwaua majambazi  watatu na kufanikiwa kukamata silaha moja aina ya bastola iliyofutwa namba, pamoja na magazine iliyokuwa na risasi moja.

Silaha aina ya Bastola.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 20, 2020, na Jeshi hilo imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 19 majira ya 7:30 mchana, maeneo ya Magomeni wakati polisi wakiwa katika doria zao za kila siku, walianza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao baada ya kuhisi wanafuatilia na ndipo walipoanza kujibu mapigo na kuwazidi nguvu.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa majambazi hao, wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salam na Mikoa ya jirani.