Jumanne , 11th Dec , 2018

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza operesheni ya kuwakamata baadhi ya watumiaji wa vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda kwa kosa la kutumia barabara ya magari yaendayo haraka ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa vifo vya raia wawili ambao waligongwa

Baadhi ya Madereva bodaboda

 gari ya mwendokasi.

Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamanda Lazaro Mambosasa ikiwa ni siku tatu zimepita tangu kutokea kwa ajali hiyo ambapo dereva wa bodaboda aliligonga basi hilo na kusababisha ajali iliyopelekea vifo vya abiria wawili eneo la Manzese Tiptop.

"Tunawashikiria madereva 20 kwa kuharibu basi la mwendokasi kwenye tukio lililotokea disemba 8 mwaka huu, niendelee kutoa onyo kwa madereva wa bodaboda kuhusu suala la matumizi ya barabara isiyokuwa kihalali," amesema Kamanda Mambosasa.

"Huyu dereva amejitakia kifo, kitendo cha kuingia kwenye barabara ya mwendokasi ni kujihatarisha maisha yake mwenyewe, kila mmoja aheshimu sheria za nchi na kila mmoja afuate taratibu za nchi na kwa jinsi tulivyojipanga hatutamuacha yeyote akivunja sheria," ameongeza Mambosasa.

"Yeyote ambaye ataendelea kupima nguvu yetu Kanda Maalum ya Dar es salaam haipimwi, bali ataishia kwenye mikono ya dola kama walivyo wahalifu wengine".

Pikipiki iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo imesajiliwa kwa namba T- 155 DCW ambapo baada ya tukio hilo baadhi ya madereva wa bodaboda waliokuwa kwenye eneo la ajali walianza kulishambulia gari la mwendo kasi na kusababisha uharibifu wa kioo cha mbele.