Polisi Mwanza yatoa neno kuhusu pesa bandia

Jumatano , 5th Dec , 2018

Watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kosa la kukutwa na noti bandia zenye thamani ya shilingi 2,830,000 pamoja na vifaa mbalimbali vya kutengenezea fedha hizo katika mtaa wa kiloleli B kata ya nyasaka wilayani ilemela, kitendo ambacho ni kosa la jinai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amesema kwa ushirikiano na maafisa wa TANAPA wa wilaya ya Serengeti, pamoja na askari wa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza, kigoma, Shinyanga, Simiyu na Mara waliweza kuwakamata watuhumiwa hao.

Shanna amesema Operesheni maalum ilifanywa na askari wa mikoa hiyo ilichukua takribani masaa 48 na kufanikiwa kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na vifaa wanavyotumia kutemgenezea noti bandia

Aidha Kamanda Shana amewatahadharisha wananchi wa Mkoa wa Mwanza kuwa makini na fedha za watuhumiwa hao ambazo tayari zipo kwenye mzunguko.

Jeshi la polisi linaendendelea na mahojiano na watuhumiwa hao watano na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili, huku msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotoroka bado unaendelea katika maeneo yote ya jiji la Mwanza na mikoa ya jirani.