Polisi yauwa watano

Wednesday , 18th Oct , 2017

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya DSM Mambosasa amesema jumla ya watuhumiwa watano wamefariki dunia baada ya kutokea majibizano ya silaha kati ya polisi na majambazi hao katika maeneo ya Msogola wilaya ya Ilala pamoja na eneo la Zakhem Kibonde Maji.

Kamanda Mambosasa amesema tukio la kwanza limetokea eneo la Msongola ambapo watu watatu waliokuwa wamepanda pikipiki iliyokuwa haina namba za usajili walipo waona askari wa doria walikimbia na kurusha silaha ndipo askari walijibu mashambaulizi na kuwauwa na katika eneo hilo walikuta SMG moja na risasi 16 na magruneti ya mikono 10.

Aidha kamanda Mambosasa amesema katika tukio lilotokea Zakhem Kibonde Maji askari walipata taarifa juu ya uvamizi wa maduka ya Mpesa ambapo watuhumiwa waliokuwa wamepanda pikipiki walipowaona askari walirusha risasi na katika majibizano watuhumiwa wawili walifariki dunia na mmoja alifanikiwa kutoroka katika eneo la tukio polisi walikuta silaha aina ya Pisto.