Ijumaa , 20th Apr , 2018

Mfalme Mswati wa Swaziland ambaye hapo jana ameadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwake, ameipa jina jipya nchi ya Swaziland na kuita 'eSwatini'.

Mfalme Mswati ametoa taarifa hiyo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza, na kusema kwamba nchi hiyo sasa itakuwa inaitwa eSwatini ikimaanisha 'Sehemu ya Swazi'.

Mfalme Mswati amefafanua kwamba mara nyingi mtu wa Swaziland akienda nje ya nchi yao hufananishwa nchi yao na Switzerland.

Kitendo hiko kimeonekana kutofurahiwa na baadhi ya watu wa Swaziland wakisema kuwa Mfalme alitakuwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi wa nchi hiyo, na sio jina la nchi.

Jina la eSwatini lilishawahi kusikika likitamkwa na Mfame Mswati kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017, na kwenye hotuba yake alipokuwa akizindua Bunge la nchi hiyo mwaka 2014.