Ijumaa , 17th Aug , 2018

Aliyekua Rais wa Uruguay Jose Mujica, aliyejulikana kama rais masikini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama Seneta.

Aliyekua Rais wa Uruguay Jose Mujica.

Mujica aliacha kazi ya useneta mnano Jumanne, wiki hii kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumu kama raisi ulipokamilika mwaka wa 2015. Amedai kwamba, amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020.

Mujica ambaye ni muasi wa zamani wa mlengo wa kushoto mwenye miaka 83, aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti, akisema, fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.

Hata hivyo, amesema, ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya kazi, mwaka 2016, alidai Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi.

Jose Mujica, almaarufu ‘Pepe’, ambaye aliwahi kuwa mpiganaji wa msituni, ambaye muda wote amekuwa akiishi katika shamba lake alikuwa akitoa sehemu ya mshahara wake kwenye shirika la misaada, ambapo aliachia madaraka baada ya kutawala miaka mitano kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.