Jumanne , 25th Feb , 2020

Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91 Jijini Cairo.

Hayati Hosni Mubarak

Mubarak aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 30 kabla ya kuondolewa madarakani kwa maandamano ya wananchi Februari 2011, amaandamano yaliyojulikana kama 'Arab Spring'.

Inaelezwa kuwa Mubarak alifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwezi Januari katika hospitali ya kijeshi Jijini Cairo kwa mujibu wa taarifa ambayo ilitolewa na mwanaye wa kiume.

Hosni Mubarak alizaliwa mwaka 1928, alijiunga na jeshi la anga la Misri akiwa kijana na kufanikiwa kuongoza vita vikubwa mwaka 1973 kati ya ukanda wa arabuni na taifa la Israel. Alikuwa Rais wa Misri miaka michache baada ya vita hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi, Anwar Sadat.

Utawala wake ulilalamikiwa kuwa na ukosefu mkubwa wa ajira, umasikini na rushwa, na kupelekea maandamano makubwa mwezi Januari 2011, ambapo baadaye alizalimishwa kujiuzulu.