Rais ataja vitu vinavyowaharibu wanaume

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Fatma Karume amefunguka kuwa kinachowaharibu wanaume huwa ni pesa na madaraka na si kingine, wengi wao hugeuka na kuanza kufanya vitendo vya kikatili.

Mwanaume akipigana na mwanamke.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa 'twitter' ameandika kuwa, "Vitu viwili vinamharibu mwanaume dhaifu: PESA NA MADARAKA. Akishayapata hayo mawili anapofuka macho na anakua kiziwi ispokua pale anaposifiwa tu".

Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa mwanamke mmoja katika kila wanawake watatu katika maisha yake amewahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia ama kimwili, kingono na kisaikolojia.

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Fatma Karume.

Ukatili wa kijinsia umegawanyika katika makundi mbalimbali ikiwemo ukatili wa kimwili, ukatili wa kisaikolojia, ukatili wa kingono, ukatili utokanao na mila na desturi, ukatili wa kiuchumi,    na ukatili wa kijinsia sehemu za kazi.

Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea ukatili wa kijinsia ikiwemo, mifumo ya jamii isiyozingatia usawa baina ya wanawake na wanaume, wanawake kutokuwa na sauti na ushiriki kwenye vyombo vya maamuzi ndani ya jamii na mitazamo hasi ya wanajamii kwa wanawake, pamoja na mfumo dume kwenye jamii.