Jumapili , 10th Nov , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). Uteuzi huu umeanza Novemba 9, 2019.

Rais Magufuli na Prof. Shadrack S. Mwakalila

 

Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Alexander Lugatona Kyaruzi, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kyaruzi anaingia katika kipindi cha pili katika nafasi hiyo baada ya kile cha kwanza kumalizika.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board). Haule pia anaingia katika kipindi chake cha pili cha uongozi baada ya kile cha kwanza kumalizika.

Rais Magufuli amemteua Dkt. Felician Bakamaza Kilahama, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Anaendelea katika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili sasa baada ya kile cha kwanza kumalizika.

Rais Magufuli amemteua Prof. Shadrack S. Mwakalila kuwa mkuu wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Memorial Academy) kuanzia Novemba 8, ikiwa ni katika kipindi chake cha pili kufuatia kile cha kwanza kumalizika.