Alhamisi , 14th Feb , 2019

Mawaziri nane kupitia timu iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa ajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi hususani katika maeneo ya hifadhi imewasili mkoani Morogoro kwa lengo la kushughulikia migogoro hiyo.

Akizungumza sababu ya ziara hiyo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi amesema kuwa mara baada ya Rais magufuli kuzuia zoezi la kuwaondoa wananchi katika maeneo ya hifadhi hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa.

Miongoni mwa hatua hizo ni kuundwa ka Kamati ya Mawaziri nane kwaajili ya kushughulikia maswala hayo ikizihusisha Wizara ya Tamisemi, Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ulinzi pamoja na Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais mazingira.

Wakiwa katika bwawa la Mindu Mawaziri wamepokea taarifa ya zoezi la kuwaondoa wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 500 kutoka katika bwawa hilo lililotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii ambapo taarifa hiyo ikamlazimu Waziri lukuvi kusitisha zoezi.