Jumapili , 6th Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameonesha kushangazwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa George Kyando, kutotekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Kangi Lugola, ambaye aliagiza kuhamishwa kwa Maaskari 9, katika kituo cha Polisi

mkoani humo.

Rais Magufuli ameonesha hali hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Rukwa, ambapo pia alikuwa akizindua mradi wa barabara kutoka Tunduma kuelekea Sumbawanga na kudai  kuwa mkoa huo unachangamoto ya masuala ya ulinzi.

"Mimi nadhani hapa Rukwa kuna tatizo kuhusu suala la ulinzi haiwezekani mtu anaachiwa hivihivi, halafu wewe RPC daah mambo mengine naomba tumwamchie Mungu." amesema Rais Magufuli.

Awali maongezi baina ya Rais Magufuli  na RPC Kyando yalikuwa hivi.

JPM : Polisi 9 walioamuliwa na Waziri kuhamishwa wameshahamishwa?
RPC - Maaskari 9 sijapata majina yao.
JPM : Alizungumza kwenye vyombo vya habari.
RPC - Niimuita OCD lakini hakuwapata.
JPM : Nimemteua anaagiza nyinyi hamtekelezi, hii ni dharau, ukatekeleze.

Tazama uzinduzi kamili hapo chin