Jumatano , 20th Nov , 2019

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kinatarajiwa kumtunikia Rais John Magufuli Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa kutokana na uongozi wake, katika ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na kuwekeza kwenye miundombinu, pamoja na kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Rais John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Makamu Mkuu wa UDOM, Prof. Faustine Bee, smesema Rais Magufuli anakuwa kiongozi watatu wa kitaifa kutunukiwa heshima hiyo ambayo .

Prof. Prof. Faustine Bee ameendelea kusema kuwa tuzo hiyo inatolewa kwa mtu aliyefanya vizuri katika nyanja mbalimbali, akitanguliwa na Rais wa Awamu ya 4, Dkt. Jakaya Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza Rashid Kawawa.

Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, amesema Rais Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kuanza ziara ya kikazi jijini humo kesho tarehe 21 hadi Novemba 25, 2019.

Katika ziara hiyo ataweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya mandeleo ikiwemo Hospitali ya Uhuru, Stendi Kuu ya mabasi pamoja na soko kuu Dodoma.