Alhamisi , 14th Feb , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Taifa kwa watu wenye ulemavu na Mwenyekiti wa wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Dkt. Lucas Luhende Kija ambaye atakuwa mwenyekiti wa baraza la ushauri la taifa kwa watu wenye ulemavu akitokea chuo kikuu kishirikishi cha elimu (DUCE) ambapo alikuwa Mhadhiri.

Mwenyekiti mpya wa bodi ya REA ni Dkt. Michael Pius Nyagoga ambaye awali alikuwa kamishna msaidizi wa Sera, Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imesema kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 13, Februari 2019.