Rais Magufuli amtaka Waziri kutumia bangi

Alhamisi , 11th Apr , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Makame Mbarawa kuwa mkali ikibidi kutumia kilevi cha bhangi, ili aweze kuwawajibisha watu zaidi.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo akiwa Makambako Mkoani Njombe ambako anaendelea na ziara yake, na kugusia sekta ya maji ambapo ndipo alipomtaka waziri kutumia kilevi hicho ambacho ni kinyume na sheria za nchi, ili aweze kuwa mkali zaidi.

Rais Magufuli akitoa maagizo kwa Waziri

"Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko, ukalisimamie hilo, kwa sababu nina matatizo sana na baadhi ya miradi ya maji, na ndio maana nimekuwa nikifanya mabadiliko kwenye miradi ya maji, kwa sababu haileti impact.  Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa, mradi umetumika milioni 400, zilikuwa milioni 800  lakini maji hayapo, sasa nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavute bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta, ili ukienda kwenye mradi hawa mainjia wa maji wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli bado yuko mkoani Njombe akiendelea na ziara yake aliyoanzia mkoani Mtwara, ambapo amezindua miradi mbali mbali ikiwemo ya barabara, vituo vya afya na viwanda, huku akiendelea kuwataka Watanzania kuchapa kazi.

Makame Mbarawa, aliyeambiwa na Magufuli akavute bangi

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Makame Mbarawa