Jumatatu , 17th Jun , 2019

Rais wa zamani wa Misri, aliyetimuliwa madarakani na jeshi mwaka 2013 Mohammed Morsi, amefariki dunia ghafla akiwa mahakamani, leo Juni 17, 2019 ambapo alikuwa amehudhuria kesi yake.

Mohammed Morsi alipokuwa gerezeni.

Kwa mujibu wa runinga ya taifa ya Misri, Morsi alifika mahakamani akiwa amefunikwa kitambaa cheusi, ambapo muda mfupi baadaye alianguka na kufariki dunia hapo hapo.

Taairifa ya Television hiyo, imeeleza kuwa mwili wa Morsi umepelekwa hospitali kwaajili ya uchunguzi zaidi na baadaye kuhifadhiwa.

Mohammed Morsi alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa kidemokrasia nchini Misri mwaka 2012 baada ya nchi hiyo kuongozwa kwa muda mrefu na mtawala wa zamani Hosni Mubarak aliyeondoka madarakani mwaka 2011. 

Mwaka mmoja baadaye mnamo 2013, akaondolewa madarakani kwa mapinduzi ya jeshi, kufuatia maandamano makubwa ya raia, kupinga utawala wake ambapo alifunguliwa mashtaka dhidi ya makosa ya uharifu wa kibidamu na ugaidi.

Morsi alikumiwa kifo akilaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo, lakini Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mwaka 2016 hivyo rufaa yake ikaendelea kusikilizwa hadi leo kifo kilipomkuta.