"Rais JPM atalishangaza Taifa" – Kingu

Friday , 19th May , 2017

Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu amesema ndani ya miaka michache ijayo Rais Magufuli atakwenda kulishangaza taifa kwa kujenga Tanzania ya viwanda japokuwa Wabunge wa upinzani wamekuwa wakiikosoa serikali bila kushauri nini kifanyike.

Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu

Elibariki alibainisha hayo pindi alipokuwa anatoa mchango wake mfupi mbele ya Bunge, wakati wa uwasilishaji bajeti ya viwanda na kudai hotuba ya kambi pinzani imejaa malalamiko mengi ambayo mengine yanasema serikali ya awamu ya tano ni ngumu kufikisha ndoto za Tanzania ya viwanda.

“Hotuba ya kambi pinzani wamesema serikali ya Chama cha Mapinduzi imechoka kiakili na uwezo wa kufikisha ndoto za Tanzania ya viwanda ‘is impossible’ …Kilichojaa kwenye hotuba ya kambi ya pinzani ni malamiko hakuna ‘alternative’ ni nini kifanyike katika mustakabali wa nchi…Ukisoma kitabu cha Mhe. Mwijage kuanzia mwanzo mpaka mwisho amejikita kwenye ‘programu, Plan, Strategy’ na namna ya 'industrialize'  nchi…Kama ni watu waliochoka akili ‘is opposition camp’ ambao kimsingi ‘this is nothing absolute nothing’ malalamiko mwanzo mpaka mwisho...Mhe. Naibu Spika kama nilivyosema wengi wanapuuza mikakati ya serikali yetu ya awamu ya tano katika kui-industrialize nchi lakini nataka nikuhakikishie ndani ya miaka michache ijayo Rais John Pombe Magufuli anakwenda kuli-suprise taifa kwa kuhakikisha kwamba Tanzania ya viwanda inakwenda kujengwa". Alisema Kingu

Pamoja na hayo, Mbunge huyo amesema watu ambao wanatega masikio wakifikili kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli itashindwa kufanikisha yale waliyoahidi kuhusu viwanda kuwa imekula kwao.