Alhamisi , 14th Mar , 2019

Sakata la kuzuka kwa maradhi ya tumbo na kuhara kwa wakazi wa baadhi ya kata za jiji la Arusha limechukua sura mpya baada ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kusema halihusishwi moja kwa moja na tatizo la maji.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Kauli hii inatolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye alilazimika kufanya ziara rasmi katika maeneo yaliyo na tatizo hilo ambapo aliongozana na wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha pamoja na Kamati ya Usalama ya Mkoa.

Amesema kupitia uchunguzi wa kimaabara bado haujathibitisha kuwa tatizo la kuhara na maradhi ya tumbo yalitokana na vimelea vya maji taka.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa na wataalamu hao walikunywa maji hayo yanayodaiwa kuwa chanzo cha maradhi moja kwa moja kutoka kwenye bomba, ambapo baadhi ya wananchi kutoka maeneo yaliyo kumbwa na adha hiyo walitoa malalamiko yao juu ya sakata hilo.

Wiki iliyopita tatizo la maradhi ya tumbo na kuhara lilizua mjadala mkali hasa katika mitandao ya kijamii na kuzua taharuki kubwa.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.