Jumatatu , 24th Sep , 2018

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amezungumzia kauli ya Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kuwa alivaa viatu mara ya kwanza baada ya kuruhusiwa kwenye mafunzo ya jadi kwa wanaume (jando) na kusema kauli hiyo inawajuza watu kuwa baba yake alifanya kazi kwa kujituma na kufikia mafanikio.

Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (kulia), akiwa na mwanaye Ridhiwani Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze.

Kauli ya Ridhiwani Kikwete imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Kikwete azindue usomaji wa kwanza wa kitabu chake alichokipa jina la safari ya kutoka shule bila viatu hadi Urais uzinduzi uliofanyika katika chuo kikuu cha Newyork nchini Marekani ambapo alitoa wito kwa wazazi pia kuwaunga mkono watoto wao kutimiza malengo yao.

Ridhiwani amesema " Ndo ukweli wenyewe huo, tukio hilo lazima watanzania wajue hakuna mafanikio yasiyokua na mapungufu yake, msione watu wamevaa vizuri na wana mafanikio watu wakaanza kusema ameiba lazima wafate historia wajue walipotokea na sio kuongea ongea bila msingi."

Mapema wiki hii Rais mstaafu Kikwete alisema "Nilipata viatu (raba) kwa mara ya kwanza  nilivyotoka jandoni ,nilikwenda navyo shule mwalimu akanambia kesho usije na viatu kila mtu hana viatu humu, kitu muhimu nachowashauri wazazi wawasaidie watoto wao kusoma, na watoto watimize wajibu wao wa kusoma.