RPC asimulia mwanzo mwisho, jinsi mtu alivyouawa

Jumanne , 5th Feb , 2019

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike, amesimulia jinsi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Pius Luhende, alivyosababisha kifo cha raia mmoja baada ya kumvamia akiwa kanisani.

Akizungumza na ww.eatv.tv, Kamanda Njewike amesema kwamba Mkurugenzi huyo alivamia kanisa akiwa na askari wa wanyama pori baada ya kuwepo kwa malalamiko ya kuharibu mali, na kwamba baadhi ya watuhumiwa walikuwa kanisani hapo.

Kamanda Njewike amesema mpaka sasa watu saba wanashikiliwa kwa mauaji hayo, na uchunguzi wa kipolisi bado unaendelea ili kuweza kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.

Sikiliza hapa chini